Vigezo na Masharti ya Matumizi
Ilisasishwa Mwisho: Agosti 2026 | Toleo 2.1
1 Utangulizi na Kukubali Vigezo
Karibu Maskani360 ("Jukwaa", "sisi"). Kwa kufungua akaunti, kuingia au kutumia huduma zetu kupitia tovuti au mfumo wetu wa kidijitali, unakubali kufungwa na Vigezo na Masharti haya. Ikiwa hukubaliani na sehemu yoyote ya vigezo hivi, tafadhali usitumie mfumo huu.
2 Aina za Watumiaji na Wajibu Wao
Maskani360 inahudumia makundi matatu makuu ya watumiaji kupitia Mfumo wa Akaunti na MASKANI ID:
- Mpangaji (Tenant): Mtu binafsi anayetafuta nyumba au eneo la kupanga. Anawajibika kutoa taarifa za kweli wakati wa kuomba kupanga au kupanga ziara.
- Mwenye Nyumba (Owner): Mtu binafsi au kampuni inayotangaza nyumba/mali zake. Anawajibika kuhakikisha mali ipo kweli, picha na bei ni sahihi, na ana haki ya kisheria ya kuipangisha.
- Wakala / Dalali (Agent): Mtu anayesaidia kuunganisha Wamiliki na Wapangaji. Anapaswa kufanya kazi kwa uaminifu, kufuata sheria za nchi, na kutowatoza watumiaji ada zisizo halali au za kitapeli.
3 Usajili na Usalama wa Akaunti (MASKANI ID)
Ili kutumia huduma kamili za Maskani360, lazima ujisajili na kupata MASKANI ID ya kipekee.
- Unawajibika kulinda nenosiri (password) lako na kutoshirikisha mtu mwingine yeyote.
- Akaunti yoyote iliyosajiliwa kwa taarifa za uongo au za kitapeli itafungwa au kuzuiliwa (Blocked) mara moja bila taarifa.
- Lazima uwe na umri wa angalau miaka 18 kisheria ili kuunda akaunti na kuingia mikataba ya upangaji.
4 Huduma za AI Assistant, Trust Score & Verified Visit
Jukwaa letu linajumuisha teknolojia za kisasa zilizoundwa kuongeza usalama na urahisi:
• Alama ya Uaminifu (Trust Score): Kipimo kinachotokana na tathmini ya taarifa za tangazo, marejesho ya watumiaji na uhakiki wa timu yetu.
• Verified Visit (Ziara Iliyothibitishwa): Mfumo wa kupanga miadi ya kukagua nyumba kwa usalama kupitia kalenda na maoni ya uhakika.
5 Kanusho la Udhamini na Ukomo wa Dhima
Maskani360 ni jukwaa la kidijitali linalokutanisha pande husika. Ingawa tunafanya kila juhudi kuhakikisha usalama kupitia *Trust Score* na *Verified Visit*, Maskani360 haitawajibika moja kwa moja kwa matatizo ya mikataba au migogoro ya kisheria inayotokea binafsi kati ya Mpangaji, Mwenye Nyumba au Wakala nje ya Mfumo wetu.
6 Kuzuia na Kufuta Akaunti
Tuna haki ya kusimamisha au kufuta Akaunti/MASKANI ID ya mtumiaji yeyote atakayebainika kukiuka sheria, kutuma matangazo ya uongo, kujaribu utapeli au kukiuka masharti haya.